Saturday 29 November 2014

Syria:Mashambulizi yashindwa kukabili IS

Waziri wa mashauri ya kigeni nchini Syria amesema kuwa mashambulizi ya miezi miwilli yanayoongozwa na Marekani yameshindwa kulidhoofisha kundi la Islamic State.
Akizungumzia kupitia kituo kimoja cha runinga nchini Lebanon Walid al-Moualem amesema kuwa njia pekee ya kukabiliana na wanamgambo hao ni kuilazimisha Uturuki kuweka ulinzi mkali kwenye mipaka ili kuwazuia wapiganaji wa kigeni kutoingia nchini humo.
Bwana Moualem alishutumu wito wa Uturuki wa kutaka kuwepo kwa eneo ambalo ndege haziruhusiwi kuruka kaskazini mwa Syria akisema kuwa hatua kama hiyo itaigawa nchi.
Kundi la wapiganaji wa IS linadhibiti maeneo makubwa ya Syria na taifa jirani la Iraq.
Mwandishi wa BBC Jim Muir amesema kuwa mshambulizi hayo ya angani yamekuwa yakisaidia zaidi katika kuwazuia wapiganaji wa IS kufika katika mpaka wa mji wa Kobane kazkazini mwa Syria.