Mwandishi
maarufu wa Kirusi Leo Tolstoy alianza riwaya Anna Karenina kwa maneno haya:
“Familia zenye furaha zote zinafanana; kila familia isio na furaha inakuwa
haina furaha kivyake.” 1 Ingawaje mimi sina hakika ya Tolstoy kwamba furaha ya
familia zote zinafanana, nimetambua kitu kimoja ambacho familia zote ni sawa
sawa: zina njia ya kusamehe na kusahau upungufu wa wengine na kutafuta wema.
Wale
walio katika familia zisizo na furaha, kwa upande mwingine, mara nyingi wanaona
makosa, wanakuwa na kinyongo, na hawaonekani kusahau makosa yaliyopita.
“Ndio,
lakini” anza na wale wasio na furaha. “Ndio, lakini haujui jinsi anavyoniumiza
mimi vibaya,” asema mmoja. “Ndio, lakini haujui jinsi huyu alivyo mbaya.” asema
mwingine.
Labda
wote ni sahihi; lakini hakuna yeyote.
Kuna
viwango vingi vya makosa. Kuna viwango vingi ya uchungu. Lakini kile nimeona ni
kwamba kila mara tunahalalisha ghadhabu yetu na kuridhisha dhamiri zetu kwa
kujiambia wenyewe hadithi kuhusu dhamira za wengine ambazo zinashutumu matendo
yetu kama yasiweza kusameheka na ubinafsi, hali wakati huo huo, tukikweza
dhamira zetu kama halisi na maasumu.
Mbwa
wa Mwana Mfalme
Kuna
hadithi ya kale ya Kiwelishi kutoka katika karne ya 13 kuhusu mwana mfalme
ambaye alirudi nyumbani na kumpata mbwa wake hakitiririkwa na damu usoni mwake.
Huyu mtu akakimbia ndani na, kwa kushituka, akaona kwamba mvulana mchanga wake
hakuwepo na susu yake ikiwa umependuliwa. Kwa ghadhabu mwana mfalme akauchomoa
upanga wake na kumuua mbwa wake. Muda mfupi baadaye, akasikia kilio cha mwanawe—mtoto
alikuwa hai! Kandoni mwa mtoto mchanga alilala mbwa mwitu aliyekufa. Yule mbwa,
kwa kweli, alikuwa amemlinda mtoto wa mwana mfalme kutoka kwa mbwa mwitu
muuaji.
Ingawaje
hii hadithi ni ya tamthiliya, inaonyesha jambo fulani. Inaonyesha uwezekano
kwamba hadithi hii unatuambia kuhusu kwa nini wengine wanatenda kwa njia fulani
kila mara haiambatani na sababu—ambazo wakati mwengine sisi hata hatutaki kujua
sababu. Tungependa afadhali tuhisi kujihalalisha wenyewe katika ghadhabu yetu
hata kwenye uchungu wetu na maudhi. Wakati mwengine hiki kinyongo kinaweza kuwa
kwa miezi au miaka. Wakati mwengine kinaweza kuwa kudumu maisha.
Familia
Iliyogawanyika
Baba
mmoja hakuweza kumsamehe mwanawe kwa ajili ya kupotoka kutoka kwa njia
aliyokuwa amemfunza. Huyu mvulana alikuwa na marafiki ambao baba yake
hakupendelea, na alifanya mambo mengi kinyume na kile baba alifikiria alifaa
kufanya. Haya yalileta ugomvi kati ya baba na mwana, na huyu mvulana punde
alipojiweza, alihama nyumbani na asirudi kamwe.
Hawakuongeleshani
tena.
Je!
Huyu baba alihisi kujihalalisha? Labda
Je!
Huyu mwana akihisi kujihalalisha? Labda
Baba, Mama na watoto
Yote
ninayojua ni kwamba hii familia iligawanyika na haikuwa na furaha kwa sababu
baba wala mwana hakuweza kusamehe mwenzake. Hawangeweza kuona zaidi ya kumbukumbu
chungu walizokuwa nazo kuhusu kila mmoja. Walijaza mioyo yao na ghadhabu badala
ya upendo na msamaha. Kila mmoja alijinyima nafasi ya kuathiri maisha ya
mwenzake kwa wema. Mgawanyiko kati yao ulionekana kuwa wa kina na mpana sana
kwamba kila mmoja akawa mfungwa kiroho katika kisiwa chake mwenyewe cha mhemko.
Kwa
bahati nzuri, Baba yetu wa Milele aliye Mbinguni mwenye upendo na hekima
alifanya njia ya kushinda ufa huu wa kiburi. Upatanisho mkuu na usio na mwisho
ni tendo kuu la msamaha na suluhu. Uzito wake ni zaidi ya uelewa wangu, lakini
nashuhudia kwa moyo na nafsi yangu yote juu uhalisi na uwezo wake wa msingi.
Mwokozi alijitoa Mwenyewe kama fidia ya dhambi zetu. Kupitia Kwake sisi
tunapata msamaha.