Friday 31 May 2013

JESHI LA POLISI NA AJIRA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU

                   TANGAZO LA AJIRA
Jeshi la Polisi Tanzania katika mwaka wa fedha 2013/2014 litaajiri vijana kutoka katika makundi yafuatayo: waliomaliza kidato cha nne mwaka 2012, kidato cha sita mwaka 2013, JKT/JKU mwaka 2013 na vyuo vya elimu ya juu mwaka 2013.Taratibu zinakamilishwa ili waliomaliza kidato cha nne na sita na waliojaza fomu za maombi kabla ya kumaliza mitihani yao ya mwisho waitwe kwenye usaili. Usaili wa vijana wa JKT umekamilika mapema mwezi Aprili, 2013.Tangazo hili linawaalika vijana walioko kwenye vyuo vya elimu ya juu nchini watakaohitimu masomo hivi karibuni na wanaopenda kujiunga na Jeshi la Polisi kujaza fomu za maombi zinazopatikana kwenye tovuti ya Polisi kwa anuani www.policeforce.go.tz Fomu za waombaji baada ya kujazwa kikamilifu ziletwe na mkuu wa chuo kabla ya tarehe 30/6/2013 kwa:
Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P. 9141,
DAR ES SALAAM.
Fani zinazotakiwa ni; Shahada za Menejimenti ya Rasilimali watu, Utawala, Uchumi, Usimamizi wa Sheria na Utekelezaji(BaLE), Ualimu, Sosholojia, Saikolojia na Ushauri Nasihi(Educational Psychology and Councelling),Takwimu, Lugha(Kiswahili/Kiingereza/Kifaransa/Kireno/Kiarabu), Usimamizi wa Programu za Maendeleo ya Jamii, Uhusiano wa Kimataifa, Uhandisi Mitambo(Mechanical Engineering), Uhandisi Kompyuta(Net Work, System Analyst, Data Base, Electronic & Telecommunications), Uandishi wa Habari, Mawasiliano ya Umma, Upangaji na Uendeshaji miradi, Jinsia na Watoto. Pia stashahada katika Usimamizi wa programu za maendeleo ya Jamii, Utunzaji kumbukumbu na Ukutubi.
Sifa za Muombaji:
  • Awe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Awe na umri usiozidi miaka 28.
  • Awe na tabia njema.
  • Awe hajawahi kushtakiwa kwa kosa la jinai.
  • Awe na afya njema.
  • Awe hajaoa/hajaolewa au kuwa na mtoto.
  • Awe tayari kufanya kazi popote ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Asiwe na alama za kuchora mwilini(Tatuu).
  • Awe hajawahi kutumia madawa ya kulevya na
  • Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya Polisi.
Imetolewa na:
Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P. 9141,
DAR ES SALAAM.

"ULIYE NAE ANAKUPENDA KWA DHATI"..

                                           Peter Chistopher katika  tafakari ya maisha

Safari ya maisha sisi kama vijana ni ndefu sana katika kufikia malengo tuliyojiwekea. Tujiulize maswali haya; nani ni msaada wangu kwa sasa? ni wakati gani msaada ninaupata? JE NINAUPATA kwa muda husika? na ni kwa namna gani? kwanini yeye kuliko mwingine? anatofautiana na wengine kiasi gani? nipo tayari kutimiza wajibu wangu? LAZIMA YEYE?
    
Maswali haya yaweza kuwa mwongozo katika kufikia malengo yetu japo yanahitaji kufikiliwa zaidi kwa kutumia fikira tunduizi na upembuzi yakinifu .
 NINGETAMANI......................................................harafu... akatokea..Itaendelee......

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YAVUNA TENA











       





WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI Dr. SHUKURU KAWAMBWA

 Matokeo ya kidato cha nne yametoka leo bado yamezidi kuzua mapya baada ya Baraza la Mitihani nchini (Necta) kulazimika kutumia kanuni iliyofanya ufaulu upande kwa asilimia tisa kutoka 34 wa awali, lengo likiwa ni kuepusha watahiniwa waliokuwa wamefaulu mwanzo kufeli.
Kanuni iliyokuwa imetumika mwanzo, ilifanya matokeo hayo yapande kwa asilimia kati ya 20 na 23, kiwango ambacho Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete aliwaeleza wabunge wa chama chake Mei 19, mwaka huu mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, wiki iliyopita maofisa wa wizara na taasisi zake wakiongozwa na Waziri Dk Shukuru Kawambwa, walijadili matokeo hayo.
 “Wakati yakijadili, ufaulu bado ulikuwa kulekule kwenye zaidi ya asilimia 54, kutokana na kanuni hiyo wanafunzi kama 2,500 waliokuwa wamefaulu kwa madaraja ya juu walikuwa washuke,” kilisema.
Kutokana na hali hiyo, kwa sasa ufaulu ni asilimia 43 jambo linalofanya matokeo hayo yawe chini ikilinganishwa na mwaka 2011.
Chanzo chetu kilieleza kuwa, katika kikao hicho, kulikuwa na mvutano kuhusu kanuni ipi itumike ili kuwaokoa wanafunzi hao alama zao zisishuke.
Baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Necta ilienda tena kuyafanyia kazi matokeo hayo ambapo sasa ufaulu umeshuka kwa asilimia zaidi ya 20 hadi kufikia  asilimia tisa.
“Kwa sasa hakuna mtu ambaye matokeo yake yameshuka, ila bwana kazi ipo siyo kama ambavyo watu wanaona kuna vurugu kweli,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Ukijaribu kuangalia, Necta wanasimamia kanuni, lakini wakati mwingine inabidi mtu uangalie hali ilivyo, kwa sasa watu wanaangalia zaidi mwitikio wa wananchi utakavyokuwa haya matokeo yakitangazwa badala ya kuangalia vitu vya msingi,” kilisema chanzo hicho.

Thursday 30 May 2013

SAFARI YAJA KWA MAFANIKIO

Ilikuwa ni ngumu kuamini kama safari hiii itafika salama kwa sababu ilijaa kila aina ya changamoto katika kufikia malengo husika zaidi niliyojiwekea. Ninamshukuru Mungu kwani.................

"UNIVERSITY LIFE"

Chrsitopher
     HAYA NDO MAISHA YANGU KAMILI HAPA CHUO.,,,.., .....

Tuesday 28 May 2013

Mbunge CCM amkacha Pinda

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipewa maelezo na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Ndile (kushoto) alipokwenda kuangalia jengo la Mahakama ya Mwanzo Mitengo mjini Mtwara, jana. Jengo hilo lilichomwa moto na watu wasiojulikana katika vurugu zilizotokea mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia.