Ili
kuwa na uhusiano wenye amani kuna mambo muhimu ya kufanya. Kwani katika
mahusiano kuna changamoto nyingi sana unaweza kukuta kile
anachokizungumza mwenza wako akiwa na wewe huku akikuonyesha mapenzi
motomoto, na ukafikiri kuwa unapendwa kuliko kitu chochote lakini kumbe
akitoka nje anatenda mambo mengine tofauti na mabaya kabisa.
Kama
kweli unataka amani ni vyema kujifunza kutenda mema. Tafakari na penda
kufanya yale ambayo wewe mwenyewe ukiyatenda utayafurahia.Ukweli ni
kwamba unaweza kufanya mambo kwa siri ukifikiria mwenzi wako hayajui
kumbe yawezekana anajua na yeye akaamua kufanya hivyohivyo tena kwa siri
yaani wote mkawa mnadanganyana.Hata kama mwenza wako anafanya mambo
mabaya.
Unachotakiwa kufanya ni kuendelea kumfanyia mazuri na si
kutenda mabaya kwa kulipiza kisasi, kwani unapotenda mema yule mtenda
mabaya atakosa amani na kuanza kutenda mazuri.Unapokwa katika mahusiano
unatakiwa kujiona kama mtu mwenye deni la kumpenda mwenzako daima. KILA
JAMBO LINAWEZEKANA NI MAAMUZI TU NA USHIRIKIANO BAINA YA WAPENDANAO. |