WATAFITIi
wa nchini Israel walibaini kuwa, mtu anayekunywa chai mara kwa mara ana uwezo
wa kuishi muda mrefu tofauti na yule asiyependa chai.
Aghalabu maisha ya mwanadamu yeyote yule yapo mikononi mwa muumba wake, ambaye hujua lini muda wa kuishi wa kiumbe wake utakwisha. Lakini mtindo wa maisha yetu usiojali kanuni za afya, umeonyesha kuwa ndicho chanzo cha watu wengi kuishi maisha mafupi.
Aghalabu maisha ya mwanadamu yeyote yule yapo mikononi mwa muumba wake, ambaye hujua lini muda wa kuishi wa kiumbe wake utakwisha. Lakini mtindo wa maisha yetu usiojali kanuni za afya, umeonyesha kuwa ndicho chanzo cha watu wengi kuishi maisha mafupi.
Kiwango cha maisha ya binadamu sasa kinapunguzwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi, mtindo wa maisha na mazingira, lakini wanasayansi na wataalamu wa afya wamekuja na mbinu ambazo zinatajwa kusaidia kuongeza miaka yako ya kuishi.
KUNYWA CHAI Watafiti wa nchini Israel walibaini kuwa, mtu anayekunywa chai mara kwa mara ana uwezo wa kuishi muda mrefu tofauti na yule asiyependa chai.
Chai, hasa ya kijani (green tea) ina ondoa sumu iitwayo ‘polyphenols’ ambayo husaidia mwili wako kupambana na magonjwa ya moyo. Wataalamu hao wanasema, chai iliyochemka vizuri au pakiti ya majani ya chai kukorogwa vyema katika majimoto, yafaa zaidi. Kwa kifupi, chai ikolee majani.
KUSIMAMA KWA MGUU MMOJA KILA ASUBUHI Inaweza kuonekana kuwa ni jambo la ajabu, lakini wanasayansi wamebaini kuwa kusimama kwa mguu mmoja asubuhi kunasaidia kuimarisha misuli ya mgongo, nyonga na tumbo na kuupa uwiano uti wa mgongo.
Mtaalamu wa viungo anasema, zoezi hili jepesi likifanywa kila siku, linatoa manufaa ya muda mrefu na linakukinga kuvunjika mifupa kwa urahisi hasa unapoanza kuzeeka. Tafuta marafiki sita unaowaamini Kuwa na marafiki wazuri na familia ambayo unaiamini ni siri moja kubwa ya kuishi miaka 100.
Utafiti uliofanywa na kitengo cha Maisha na Mazingira katika Chuo Kikuu cha Australia, ulionyesha kuwa kupata watu wa kukupa msaada na kukufariji wakati wa huzuni kunasaidia kuongeza umri wa kuishi kwa kuzalisha kemikali ya ‘furaha’ inayofahamika kama dopamine na oxtocyin ambavyo huusaidia ubongo.
Mwanasaikolojia wa Chuo Kikuu cha Dodoma, anasema unapokuwa na tatizo, kisha ukalihifadhi moyoni, unaunda uchungu ambao unakuathiri. Anasema, mwili wa mtu unaathiriwa kutokana na tabia au matendo ya moyoni, unapohifadhi tatizo bila kupata ushauri unakuza tatizo hilo.“Marafiki au hata ndugu wa kumweleza tatizo lako ni muhimu, wanaweza kukupoza,” anasema
USISHIBE SANA Wakazi wa kisiwa cha Okinawa, nchini Japan, wanaongoza kwa kuwa na kiasi kidogo cha watu wenye unene uliopitiliza (obesity) na wanasifika kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaoishi zaidi ya miaka 100. Siri yao kubwa ni kuwa hawali wakashiba kwa zaidi ya asilimia 80.
Watafiti wa Marekani pia, wamebaini kuwa, binadamu wanaweza kuishi miaka mingi zaidi iwapo chakula wanachokula kinapunguzwa kwa robo tatu. Ina maana kwamba kula kidogo kunaufanya mwili wako usiwe na kazi kubwa ya kumeng’enya, hivyo kuupa nafasi ya kuwajibika na kazi nyingine.
Mtaalamu wa chakula na lishe, anasema, mtu hatakiwi kula akashiba bali anatakiwa aache njaa kwa mbali ili kutoa nafasi ya maji na mmengenyo kuchukua nafasi.
LALA KWA MUDA MREFU Ukosefu wa usingizi unakuweka katika hatari kubwa ya kupata maradhi ya msongo wa mawazo na moyo. Kupata makunyanzi na mwili kuchoka.
Mabadiliko kidogo tu ya kitabia yanaweza kuleta mapinduzi makubwa katika afya yako. Wanaopata usingizi wa kutosha si rahisi kupatwa na kiharusi au shinikizo la damu.
PIGA MSWAKI
Maradhi ya fizi, ni maradhi yaliyopata umaarufu duniani. Dk James Russel wa
kituo cha tiba cha Hope, anasema, meno na fizi ni chanzo cha magonjwa mengi
ambayo wengi hudhani hayahusiani na afya ya kinywa. Maradhi ya fizi yanatajwa
kuwa chanzo cha saratani za aina fulani, maradhi ya moyo, ubongo na hata
kisukari.
KUWA
MAKINI
Utafiti uliofanywa na Mwanasaikolojia wa nchini Marekani, Dk Howard Friedman unasema kuwa, umakini wa mtu ni kigezo cha urefu wa maisha yake. Watu ambao wapo makini na maamuzi, matumizi ya fedha na ambao wanapenda kuweka kila kitu sawa na kufanya mambo yao kwa uangalifu, wanaweza kuishi kwa muda mrefu.
KWA NINI? Dk Kitila Mkumbo, Mwanasaikolojia wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) anasema, unapokuwa makini unafanya uamuzi mzuri ambayo hupunguza kiwango cha kuishi maisha hatarishi.
“Umakini unamsaidia mtu kuepuka tabia hatarishi kwa mfano ngono zembe, kuvuta sigara, mambo ambayo yanahatarisha afya,” anasema.
Anasema, mtu anayepangilia mambo yake na kuwa makini kwa mfano kutumia kinga wakati wa tendo la ndoa kunakuepusha na maambukizi ya maradhi mbalimbali.
USIWEKE MATUNDA KWENYE JOKOFU Unaweza kufikiri kuwa, kuyaweka matunda katika jokofu, unayafanya yadumu kwa muda mrefu, lakini tafiti zinaonyesha kuwa, matunda yaliyopoozwa kwa baridi ya jokofu, yanapungukiwa vitamini muhimu kuliko matunda yanayowekwa katika hali ya kawaida.
Kwa mfano, nyanya na pilili ni vyema kuwekwa katika bakuli kuliko katika jokofu. Matunda mengi yanasaidia kuondoa sumu mwilini hivyo lishe zake zikibaki bila kuharibiwa, husaidia kujenga moyo imara na kupunguza kiwango aina fulani za saratani.
KUFANYA TENDO LA NDOA ANGALAU MARA MBILI KWA WIKI
Utafiti mkubwa na uliothibitishwa wa Welsh na wenzake wa Hospitali ya Royal Edinburgh, Uingereza ulibaini kuwa wale wanaofanya mapenzi mara moja kwa mwezi wapo katika hatari ya kufa mapema, ukilinganisha na wale wanaofanya mapenzi mara mbili kwa wiki.
Welsh anasema, tendo la ndoa linapunguza msongo wa mawazo na kumfanya mtu apate usingizi mzuri. Msongo wa mawazo unasababisha maradhi ya moyo na kisukari. Dk Mkumbo anasema, tendo la ndoa ni jambo la afya na husaidia katika kupunguza msongo wa mawazo na kuupa mwili uchangamfu. Hata hivyo Dk Mkumbo anasema hajawahi kusikia idadi ya siku za kufanya mapenzi kama ni mara moja au mbili kwa wiki, bali anaamini kitendo chenyewe kina umuhimu wake kiafya.
Kwa nini Wajapan wanaishi maisha marefu? Inaelezwa kuwa Wajapan ni taifa linaloongoza kwa kuwa na watu wanaoishi muda mrefu kuliko mataifa mengine. Takwimu za Shirika la Afya Duniani zinaeleza kuwa, raia wa Japan wanaishi maisha marefu zaidi. Kwa mfano, mwanaume mzee kuliko wote aliyevunja rekodi ni Jiroemon Kimura, kutoka Kyotango, Kyotto, Japan aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 116. Siri yao kubwa ni kula chakula chenye afya ikiwemo samaki badala ya nyama nyekundu.
Hawanywi maziwa, au bidhaa zozote za ng’ombe. Nafaka jamii ya soya ambazo zinasaidia kuondoa maradhi ya moyo. Wanakunywa chai kwa wingi, hasa ya kijani, wanakula kiasi kidogo cha chakula, hawatumii magari mara kwa mara na wanatumia vyoo vya kuchuchumaa badala ya vya kukaa.
..inaonekana
hizi TAFITI zinashabiana na WATAFITIi wa hapa nchini na nje waliobaini haya:-
wataalamu na wanasayansi nchini wametaja mbinu mbalimbali ambazo binadamu akizifuata, anaweza kuishi zaidi ya miaka 100. Wataalamu hao, kutoka vitengo mbalimbali vya Sayansi ya Jamii na Viumbe hapa nchini, wamesema mtu akiishi bila kuathirika akili na mwili, anaweza kuishi maisha marefu zaidi kuliko yule anayeathirika katika vitu hivyo. Wasomi hao wamebainisha kuwa mgawanyo wa mwili, akili na roho, ni mambo muhimu katika mwili wa mwanadamu yaliyo na uwiano unaoingiliana na havitenganishik i.
Kukabili msongo wa mawazo
Akizungumza na Mwananchi Jumapili, Mtaalamu wa Saikolojia na Mkuu wa Kitengo cha Sosholojia wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Joyce Nyoni aliitaja mbinu ya kwanza ya kuongeza maisha kuwa ni kukabiliana na msongo wa mawazo. Daktari huyo alisema akili ya mtu huweza kuathiri mwili. Wengi wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na maradhi yanayotokana na msongo wa mawazo, kama vile maradhi ya moyo au vidonda vya tumbo. “Wengi wetu tuna msongo wa mawazo, jambo dogo linaweza kumfanya mtu akashindwa hata kula au kulala, ni lazima tujifunze kukubaliana na hali halisi ya maisha, huku tukiamini kuwa, hakuna jambo lisilo na utatuzi,” alisema Dk Nyoni.
Alisema wapo wanawake wengine ambao hupoteza maisha kwa sababu ya waume zao kuwatesa au kuwatelekeza. “Ni lazima tufahamu kuwa maisha hata siku moja hayawezi kunyooka, ni lazima viwepo vikwazo vya hapa na pale, kwa hiyo hatuna budi kujifunza kuzikabili changamoto za maisha,” alisema. Utafiti uliwahi kufanyika na kuonyesha kuwa, wanawake chini ya miaka 50 na walio katika kipindi cha kufunga hedhi, (menopause) ambao hawawezi kukabiliana na msongo wa mawazo, wanaugua maradhi ya moyo. Alisema yeye kama mtaalamu wa masuala ya saikolojia, huwashauri watu kutulia na kukubaliana na matokeo yoyote katika maisha.
Kuishi mfumo chanya, kucheka
Jambo
lingine ambalo mtaalamu huyu alishauri ni kuishi katika mfumo chanya. Alisema
watu wengi hawatosheki na kile kidogo wanachopata, badala yake wanaishi kwa
kulalama jambo ambalo kwa asilimia kubwa, huchangia maradhi ya moyo. “Mara kwa
mara huwa nawaeleza wanafunzi wangu, ukimwona mwanamke kavaa mikufu, bangili na
hereni nyingi masikioni, vyote vya dhahabu, huyo ni mgonjwa, kwa sababu
ukimnyang’anya au akiibiwa ujue ataugua,” alisema Dk Nyoni. Alisema, ni vyema
watu waishi kwa kuridhika na chochote wapatacho, badala ya kutoridhika na hali
yao na kutamani maisha ya wengine.
“Namthamini mwanamke anayetoka nyumbani, amechana nywele zake kawaida, amepaka mafuta, lakini anajiamini, kuliko yule ambaye anataka atazamike kuwa ni wa thamani na mwenye fedha, mbele za watu, kwa kuvaa nguo za thamani kubwa au kuendesha magari ya kifahari,” alisema .Mtaalamu huyo alitaja mbinu nyingine ya kurefusha maisha kuwa ni kucheka au kuwa na furaha
Mazoezi, usingizi wa kutosha
“Namthamini mwanamke anayetoka nyumbani, amechana nywele zake kawaida, amepaka mafuta, lakini anajiamini, kuliko yule ambaye anataka atazamike kuwa ni wa thamani na mwenye fedha, mbele za watu, kwa kuvaa nguo za thamani kubwa au kuendesha magari ya kifahari,” alisema .Mtaalamu huyo alitaja mbinu nyingine ya kurefusha maisha kuwa ni kucheka au kuwa na furaha
Mazoezi, usingizi wa kutosha
Naye Dk Nandera Mhando, wa Kitengo cha Sosholojia na Athropolojia cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema hakuna ubishi kuwa zipo tabia ambazo husababisha baadhi ya watu kukumbwa na maradhi na kufa katika umri mdogo. “Wapo ambao hawana kabisa tabia za kufanya mazoezi, hawa huwa na uzito mkubwa na miili yao inapokuwa na mafuta mengi, maradhi ya moyo huwa yamepata nyumba, lakini pia kutopata usingizi wa kutosha nalo ni tatizo,” alisema.
Tabia ya mtu, vyakula
Dk Mhando alisema, tabia ya mtu ni sababu nyingine inayoweza kumfanya mtu awe na maisha mafupi, kwa mfano, kupenda kufanya ngono, kuvuta sigara, na ulevi ni mambo yanayosababisha maradhi na kuleta kifo.
“Kama mtu tayari ameathirika, halafu anandelea kufanya ngono kwa kiasi kikubwa, si ajabu mtu huyo kufa mapema, lakini wanaokunywa pombe na kuvuta sigara kwa wingi, nao mara nyingi huugua maradhi ya figo, mapafu, ini nk.,” alisema. Daktari huyu aliongeza kwamba, aina za vyakula tunavyokula nayo vinachangia kupima afya ambayo kimsingi ni kipimo cha maisha ya binadamu.
Alisema wanaokula vyakula asilia, kama mboga za majani, kunywa maji na kula matunda kwa wingi, si rahisi kushambuliwa na maradhi, tofauti na wanaokula wanga peke yake ambao wanakuwa katika hatari ya kupata maradhi, hatimaye kifo. Imethibitishwa kuwa, Mwanabaolojia mmoja, wa nchini Marekani, Ancel Keys, hata baada ya kustaafu, aliendelea kufanya kazi za bustani nyumbani kwake kwa kiasi kikubwa jambo lililomfanya kuishi miaka 100. Alifariki mwaka 2004.
Dini
Mtaalamu wa Sosholojia ya Dini kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Thomas Mwendaluka, alisema, dini ni moja ya maeneo ambayo huweza kuchangia mtu kuishi maisha marefu.
“Dini ina pande mbili, hasi na chanya, kwa sababu kwa upande mmoja inatoa tumaini. Inamsaidia mtu kiimani kuishi maisha marefu na vilevile ni chanzo cha kufupisha maisha,” alisema Mwendaluka. Alisema, watu huweza kujengwa kiroho na kuamini uponyaji wa magonjwa yaliyoshindikan a. Kwa mfano tangu UKIMWI ulipoingia , waathirika wengi wamekimbilia katika taasisi za dini na kule hujengwa kiroho na kiimani na kujisikia wamepona na kuongeza siku za kuishi. “Lakini baadhi ya imani, kwa mfano Boko Haram, zinawataka waumini wajitoe muhanga kuua, hilo hufupisha maisha ya wengi,” alisema Mwendaluka. David Larson, Mshauri wa Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili wa nchini Marekani, alifanya utafiti wake mpana juu ya uhusiano wa moja kwa moja uliopo kati ya dini na afya.
Uchunguzi wake ulionyesha wazi kwamba upo uhusiano wa moja kwa moja kati ya muumini aliyejitoa kwa moyo katika imani husika na afya yake. Alishangaa kubaini kwamba, wale wanaohudhuria kanisani wanaishi muda mrefu kuliko wale wasiohudhuria. “Nilishangazwa kujua kuwa kutumainia uweza wa Mungu ndio msingi wa ustawi wa kweli na maisha ya afya yenye furaha,” alisema Larson.
Kunywa maji mengi
Daktari wa Kitengo cha Patholojia katika Hospitali ya Muhimbili, Innocent Mosha anasema maji ni jambo lingine linaloweza kukupa afya na kukuepusha na maradhi. “Kazi ya maji ni kusafisha ini na figo, kwa hiyo si ajabu mtu asiyekunywa maji ya kutosha akawa na afya mbaya kwa sababu uchafu hubaki katika damu,” alisema Dk Mosha. Matabibu wengi wanashauri kuachana na aina za vyakula kwa mfano, nyama ya wanyama yenye mafuta ya majimaji (saturated fat) na mafuta mazito (cholesterol), ambavyo huongeza hatari ya kupata shinikizo la damu, kupooza
(stroke), ugonjwa wa moyo, kansa, unene usio wa kawaida, kisukari na magonjwa mengineyo. Mwandishi wa kitabu cha ‘The Blue Zones’ Dan Buettner, ambaye alifanya utafiti kuhusu siri ya ya kuishi maisha marefu katika nchi za Bara la Australia, Greece na China, aligundua kuwa, watu wa nchi hizo wana tabia za kufanana ambazo bila shaka huwafanya waishi maisha marefu. Alisema wote hula milo yenye kiasi kidogo cha nyama na wanafanya mazoezi.
=============
1. Jiweke mbali na sigara.
2.
Epuka unene.
3.
Fanya mazoezi.
4.
Kula lishe bora.
5.
Hakikisha unacheki na kupima kiwango cha kolestero mwilini, shinikizo la damu
na sukari na kuhakikisha viko katika kiwango kinachotakiwa.
Uchunguzi huo umeonyesha kwamba watu wengi umri wa kuanzia miaka 50 ambao wanaishi kwa kufuata masharti hayo huwa na uwezo wa kuishi miaka 40 zaidi bila kupata shinikizo la damu na ugonjwa wa moyo, ambayo ni magonjwa makuu mawili yanayoua watu zaidi duniani. Wataalamu wamesema kwamba, kila mtu anayetaka kuishia maisha marefu anatakiwa kufuata ushauri ufuatao:
• Jiepushe kuvuta sigara au acha kuvuta sigara kabisa.
• Kila wiki pata dakika zisizopungua 150 za kufanya mazoezi ya kawaida.
• Jitahidi kufuata maelekezo ya kula lishe bora ambayo ni: vikombe 4 na nusu vya matunda na mboga mboga kwa siku, samaki mara mbili au tatu kwa wiki. Usinywe sana vinywaji vyenye sukari, kula vyakula vyenye ufumwele kila siku na chumvi isizidi miligram 1,500 kwa siku.
Uchunguzi huo umeonyesha kwamba watu wengi umri wa kuanzia miaka 50 ambao wanaishi kwa kufuata masharti hayo huwa na uwezo wa kuishi miaka 40 zaidi bila kupata shinikizo la damu na ugonjwa wa moyo, ambayo ni magonjwa makuu mawili yanayoua watu zaidi duniani. Wataalamu wamesema kwamba, kila mtu anayetaka kuishia maisha marefu anatakiwa kufuata ushauri ufuatao:
• Jiepushe kuvuta sigara au acha kuvuta sigara kabisa.
• Kila wiki pata dakika zisizopungua 150 za kufanya mazoezi ya kawaida.
• Jitahidi kufuata maelekezo ya kula lishe bora ambayo ni: vikombe 4 na nusu vya matunda na mboga mboga kwa siku, samaki mara mbili au tatu kwa wiki. Usinywe sana vinywaji vyenye sukari, kula vyakula vyenye ufumwele kila siku na chumvi isizidi miligram 1,500 kwa siku.
• Kiwango cha kolestero au mafuta katika damu yako kisizidi 200.
• Shinikizo lako la damu lisiwe zaidi ya 120 chini ya 80.
• Sukari katika damu iwe chini ya 100
Source: Jamiiforums Apr 17, 2014