Tangu tupate
Uhuru mwaka 1961, Serikali ilidhamiria kuwa na upangaji shirikishi katika
mchakato wa mipango ya kiuchumi, ili kuwa na mfumo wa upangaji unaotoka chini
kwenda juu. Juhudi za serikali za kutekeleza dhamira hii zinaweza kuangaliwa
katika hatua mbalimbali zilizochukuliwam kushirikisha Jamii katika kujiletea
maendeleo yao. Juhudi hizi zinaweza kuangaliwa katika awamu
kuu tatu:
- · Kipindi cha 1961 – 66 (Mara baada ya Uhuru)
- · Kipindi cha 1967 – 92 (Azimio la Arusha)
- · Kipindi cha 1992 – 2002 (Kipindi cha Maboresho)
Kipindi cha
tatu, 1992 – 2002 kilitawaliwa na maboresho ya sekta ya Umma. Serikali ya
Jamuhuri
ya Muungano wa
Tanzania (Bara) ilifanya maboresho kwa ajili ya kuongeza ufanisi na uwezo wa
sekta ya umma
katika utoaji huduma bora. Maboresho yamejikita katika maeneo yafuatayo:
- Maboresho ya Utumishi katika serikali kuu
- Maboresho ya serikali za mitaa
- Maboresho katika sekta ya fedha
- Maboresho katika sekta ya sheria
- Maboresho katika upangaji mipango na baajeti
- Maboresho katika mashirika ya Umma
- Maboresho ya muundo wa Tawala za Mikoa
Shabaha za
maboresho haya ni kuleta mabadiliko ya majukumu ya serikali kuu kutoka yale ya serikali
hujihusisha moja kwa moja na utekelezaji, uzalishaji mali na utoaji huduma na
kuwa yale
ya kuandaa sera,
kuratibu, kushauri, na kujenga uwezo wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, watu binafsi
na mashirika yasiyo a siserikali. Aidha, kujenga mazingira yanayowezesha
serikali na wananchi kushirikiana kuboresha utendaji wa kazi kwa upande mmoja
na serikali za mitaa kuwa na majukumu ya utekelezaji na usimamizi wa shughuli
zote za maendeleo, utoaji huduma, utawala wa kisheria na uimarishaji demokrasia
ili kurahisisha maendeleo ya wananchi.
Ingawa serikali
iliendelea kuweka mazingira mazuri ya ushirikishwaji kama ilivyoelezwa hapo juu
bado ushirikishwaji wa wananchi katika kupanga na kutoa maamuzi uliendelea
kumilikiwa na Maafisa mipango / wachumi, warasimu na wafadhili ambao wana hisia
potofu za udhibiti na
ufanisi wenye
msingi wa “tunajua (wataalamu) wao (Jamii) hawajui” kwa hiyo, Ushirikishwaji wa
wananchi katika kupanga na kutoa maamuzi haukutekelezwa kikamilifu. Huko nyuma
wananchi walihusishwa tu kwa kutumia njia zifuatazo; (1) Chakula kwa kazi, (2)
Kuchangia gharama, (3) Mikataba na walengwa.
Kumekuwepo na
majaribio mbalimbali ya kutumia mbinu shirikishi katika baadhi ya maeneo hapa nchini,
hasa katika miradi iliyofadhiliwa na wahisani. Baadhi ya mbinu shirikishi
zilizotumika katika jitihada hizi ni: PRA, SARAR, ZOOP na LEPSA.
Kwa kiwango
fulani mbinu hizi shirikishi zimewezesha Jamii kufanya maamuzi katika mchakato
wa upangaji. Hata hivyo mbinu hizi zote zilikuwa zikiegemea zaidi katika
kubaini matatizo hivyo basi kuongeza mategemeo ya Jamii kwamba watapewa misaada
mara moja kutoka nje kutatua
matatizo yao.
Hali hii inajenga tabia tegemezi, pia mara nyingi miradi ya wafadhili
inayotumia
mbinu shirikishi
inakuwa tayari inayo malengo yao tofauti na yale yanayoibuliwa na wananchi;
hivyo kutoa
nafasi ndogo sana kwa Jamii kujiamulia yale wanayotaka.
Kwa mapungufu
hayo, juhudi hizi ziliishia kwenye kuwahusisha tu wananchi badala ya kuwashirikisha,
kwa ujumla upangaji mipango nchini Tanzania umeendelea kubaki kuwa ule wa
kutoka juu
kwenda chini tofauti na mategemeo ya serikali.
Matarajio ya Serikali katika
kuimarisha upangaji yalikuwa kama ifuatavyo;-
- · Kuongeza ushiriki wa wananchi
- · Kuwa na mipango ya uwiano
- Kuwa na upangaji wa kutoka chini kwenda juu
Mfumo wa upangaji mipango
shirikishi wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo unatoa njia ambayo itasaidia
serikali kufikia matarajio haya.