Wednesday 9 November 2016

Sababu zilizosababisha Trump Kushinda


Ni wachache waliokuwa na fikra kuwa Trump angewania. Donald Trump alipita vizingiti vyote kutoka mwanzo wa kampeni yake ya kuwania urais zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Ni watu wachache walikuwa na fikra kuwa angeweza kuwania, lakini yeye alifanya hivyo. Walifikiri hangepata umaarufu lakini akafanya hivyo. Wakasema hangeweza kushinda mchujo wowote lakini akafanya hivyo. Wakasema hangeweza kushinda uteuzi wa Republican lakini akafanya hivyo.

Image result for donald trump

Majimbo yaliyokuwa ngome Democratic yalimpigia kura  Majimbo yaliyokuwa ngome Democratic yalimpigia kura Trump Kisha wakasema kuwa hakuna vile angeweza kushindana au hata kushinda na sasa ni yeye rais mteule wa Marekani.
Majimbo yaliyokuwa ngome ya Democratic yote yalimpigia kura Trump yakiwemo Ohio, Florida na North Carolina.

Trump ashinda urais Marekani
Watu wazungu walio na ajira hasa wale wasio na masomo ya chuo kikuu wanake kwa wamaume walikihama chama kwa wingi.

Donald Trump ni rais wa 45 wa Marekani

Wapiga kura wa mashambani walijitokeza kwa wingi huku Wamarekani wanaohisi kutengwa na watu wa mijini wakipiga kura kwa idadi kubwa. Wasifu wa Trump, mshindi wa urais Marekani Licha wa majimbo kama Virginia na Colorado kumchagua Clinton, jimbo la Wisconsin lilimwendea Trump na kusababisha matumaini ya Clinton kudidimia.

Trump alimdhalilisha John McCain. Akaanza ugomvi na mtangazaji wa kituo cha Fox News Megyn Kelly. Wafuasi wengi wa Democratic walihamia Republican

Wafuasi wengi wa Democratic walihamia Republican Aliomba msamaha shingo upande wakati kanda moja ya video ilitolewa, akijigamba jinsi alivyowadhalilisha kimapenzi wanawake. Alipambana na pingamizi ndani ya chama chake na kushinda zote. Trump alijenga himaya yake kutoka wa washindani wake kaiam mchujo. Wengie kama Marco Rubio, Ted Cruz, Chris Christie na Ben Carson baadaye walisalimu amri. Hatimaye Trump anaelekea ikulu ya White House

Hatimaye Trump anaelekea ikulu ya White House
Wafuasi wengi wa chama akiwemo spika Paul Riyan na wengine, Trump hakuhitaji msaada wao, na kwa uhakika huenda ameshindana kwa sababu aliamua kuchukua msimamo dhidi yao. Ted Cruz: Nimempigia kura Trump

Ni dalili ambayo wanasiasa wengine waliiona kwa mbali, Bernie Sanders na Tedd Cruz kwa mfano. Lakini hata hivyo hakuna mtu aliyeilewa kama Trump mweyewe na ndivyo ikampeleka ikulu ya White House.

Friday 8 July 2016

France Na Ureno fainali jumapili

Ufaransa imetinga katika hatua fainali ya Kombe la Mataifa barani Ulaya kwa mwaka huu baada ya kuifunga Ujerumani 2 - 0.
Mshambuliaji Antoine Griezmann ndiye aliyeipeleka timu yake ya Ufaransa katika hatua fainali ya Kombe la Mataifa barani Ulaya kwa mwaka huu baada ya kuifungia magoli 2 na kuishangaza Ujerumani iliyokuwa imetawala mchezo huo wa nusu fainali.

Mshambuliaji huyo wa Atletico Madrid alianza kwa kuandika bao la kwanza kwa njia ya penalti katika dakika ya 45 kipindi cha kwanza kabla ya kupachika bao la pili na ushindi kipindi cha pili baada ya golikipa wa Ujerumani Manuel Neuer kufanya makosa golini.
Kwa matokeo hayo sasa Ufaransa mwenyeji wa michuano hiyo itakutana na Ureno katika mechi ya fainali siku ya Jumapili