| Carles Puyol |
Nahodha
wa klabu ya Barcelona Carles Puyol ametangaza atawahama mabingwa hao wa
Hispania mwishoni mwa msimu huu. Puyol
mwenye umri wa miaka 35 aliibukia kutoka vikosi vya vijana wa Barcelona na
kujiunga na kikosi kikuu mwaka 1999.
Amewachezea
mabingwa watetezi wa La Liga takriban mara 400.
Ameshinda
vikombe sita vya ubingwa wa Ligi,vikombe vitatu vya klabu bingwa ya
Ulaya,vikombe viwili vya shirikisho la kandanda la Uhispania pamoja na vikombe
vya super cup vya klabu za ulaya na Uhispania.
Pia
amekua mchezaj muhimu katika nyanja ya kimataifa akiisaidia Hispania kunyakua
ubingwa wa bara la Ulaya mwaka 2008 na kombe la dunia miaka miwili badae.
Hata
hivyo amekua akisumbuliwa na magoti katika miaka ya hivi karibuni na hakuweza
kushiriki katika michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2012.
Msimu
huu ameichezea Barcelona mara 12 tu. Puyol,
ambae ameiwakilisha Hispania mara 100,alicheza mechi yake ya mwisho dhidi ya
Uruguay, Februari 2013.
Amesema
angependa kupumzika baada ya kuondoka Barcelona. "sijui ntakachofanya
baada ya Juni 30 lakini nina hakika nitapumzika" akaongeza.
"nitaitisha
mkutano na waandishi habari mwishoni mwa msimu huu ili niwaage baada ya
kuichezea klabu hii kwa muda wa miaka 19 ," alisema Puyol