
Atletico Madrid
Diego
Costa amedumisha rekodi ya kufunga katika mechi zake zote wa kuwania kombe la
klabu bingwa barani Ulaya, msimu huu pale Atletico Madrid ilipoishinda AC
Millan na kufuzu kwa robo fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1997.
Mshambulizi huyo,
ambaye aliifungia Madrid bao la pekee katika mechi ya raundi ya kwanza,
alivurumisha kombora kali baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Koke dakika ya
pili. Arda Turan naye alifunga la pili kabla ya Raul Garcia kuongeza la tatu.
Na ili
kudhihirisha kuwa yuko katika hali nzuri kwa sasa, Diego Costa kwa mara
nyingine tena aliliona nyafu za wapinzani wao na kufunga bao lake la pili
katika mechi mechi.
Diego Costa
Costa, ambaye
aliichezea timu ya taifa ya Uhispania mechi yake ya kwanza, amefunga magoli
saba katika mechi tano za kuwania kombe la klabu bingwa Ulaya msimu huu na
amefunga magoli 29 katika mashindano yote aliyoshiriki.
Leo usiku kutakuwa
na mechi mbili, Barcelona watakwaruzana na Manchester City nayo Bayer
Leverkusen wakisafiri Ufaransa kuchuana na Paris Saint Germain.