Jiji la Singapore
Singapore
umetajwa kuwa mji ghali zaidi duniani kuishi kwa mwaka 2014 na kuipiku miji
mingine 131 kwa mujibu wa taarifa ya Economist Intelligence Unit (EIU).
Nguvu
ya sarafu ya mji huo ikiwa ni pamoja na gharama kubwa ya uendeshaji magari na
kuongezeka kwa malipo ya huduma za umma kumechangia Singapore kuwa juu ya miji
yote duniani kwa ughali wa maisha.
Pia
ni mahali ambapo nguo zinauzwa kwa bei ya juu kabisa kuliko miji yote duniani.
Singapore
imechukua nafasi ya mji wa Tokyo, amao ulikuwa unaongoza kwa ughali wa maisha
mwaka 2013.
Miji
mingine mitano inayoongoza kwa gharama kubwa za maisha duniani ni pamoja na
Paris, Oslo, Zurich na Sydney, huku Tokyo ukiporomoka hadi nafasi ya sita.
Mji
wa New York unatumiwa kama kigezo cha utafiti wa shirika la EIU kuhusu gharama
za maisha katika miji mbalimbali duniani. Wanaangalia zaidi ya bei binafsi 400.