Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi - CCM, SHAKA HAMDU SHAKA amesema Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi - UVCCM
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi - CCM, SHAKA
HAMDU SHAKA amesema Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi - UVCCM
Kisiwani ZANZIBAR umejipanga vyema katika kuhakikisha CCM inanyakua
baadhi ya majimbo Kisiwani PEMBA katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika
mwaka huu.
SHAKA amesema hivi sasa wameanza kujipanga kuhakikisha azma yao
inafanikiwa kwa kuendelea kunadi vyema Ilani ya Chama Cha Mapinduzi
katika Kisiwa cha PEMBA.
Kuhusu uteuzi wa wagombea wa CCM ngazi ya Taifa SHAKA HAMDU SHAKA
amesema uteuzi huo umezingatia vigezo vyote vya sifa za wagombea ambao
wote wana uwezo mkubwa wa kuongoza Taifa.
Hapo jana wanaCCM ZANZIBAR walifanya mapokezi ya kupongeza uteuzi wa
nafasi ya Urais wa ZANZIBAR kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi uteuzi
ambao uliweza kupitishwa kwa asilimia mia moja na Mkutano Mkuu wa
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM huko mjini DODOMA
No comments:
Post a Comment