Wizara ya Fedha
kupitia Naibu wake Waziri wa fedha Mh. Mwigulu Nchemba wametangaza uamuzi wa
kufuta malipo ya Wabunge waliosusia vikao vya mchakato wa Katiba vinavyoendelea
Dodoma.
Uamuzi huu
umetangazwa ikiwa ni siku ya pili tangu Wajumbe wa Bunge la Katiba Kutoka UKAWA
wasusie Shughuli za Bunge la Katiba kwa Madai wamechoka matusi na Kuburuzwa
kwenye Bunge hilo.
Hii leo Naibu
waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Nchemba ambaye kwa Sasa anakaimu Kuwa Waziri wa
Fedha tangu April 10 20014 baada ya Waziri wa Fedha kupata safari
ya kikazi nchini Marekani,amefuta Malipo ya wabunge waliosusia Mchakato huo wa
Katiba.
Mheshimiwa Mwigulu
Nchemba ameagiza Benki zote kurudisha Cheque za Malipo ya Posho na seating
allowance ambazo zilipelekwa Bungeni April 16 ili ziwekwe kwenye akaunti
binafsi za Wabunge ikiwa ni Malipo ya Mpaka April 30.
Uhakika wa taarifa
hizi anazisema mwenyewe Mh.Mwigulu Nchemba kupitia Exclusive Interview na millardayo.com na kuelezea uamuzi huu pamoja na
mtazamo wake kuhusu hili bunge la Katiba linaloendelea kwa sasa.