Tuesday, 22 April 2014

Msingi Muhimu kwa Familia yenye Furaha


Mwandishi maarufu wa Kirusi Leo Tolstoy alianza riwaya Anna Karenina kwa maneno haya: “Familia zenye furaha zote zinafanana; kila familia isio na furaha inakuwa haina furaha kivyake.” 1 Ingawaje mimi sina hakika ya Tolstoy kwamba furaha ya familia zote zinafanana, nimetambua kitu kimoja ambacho familia zote ni sawa sawa: zina njia ya kusamehe na kusahau upungufu wa wengine na kutafuta wema.

Wale walio katika familia zisizo na furaha, kwa upande mwingine, mara nyingi wanaona makosa, wanakuwa na kinyongo, na hawaonekani kusahau makosa yaliyopita.
“Ndio, lakini” anza na wale wasio na furaha. “Ndio, lakini haujui jinsi anavyoniumiza mimi vibaya,” asema mmoja. “Ndio, lakini haujui jinsi huyu alivyo mbaya.” asema mwingine.
 

Labda wote ni sahihi; lakini hakuna yeyote.
Kuna viwango vingi vya makosa. Kuna viwango vingi ya uchungu. Lakini kile nimeona ni kwamba kila mara tunahalalisha ghadhabu yetu na kuridhisha dhamiri zetu kwa kujiambia wenyewe hadithi kuhusu dhamira za wengine ambazo zinashutumu matendo yetu kama yasiweza kusameheka na ubinafsi, hali wakati huo huo, tukikweza dhamira zetu kama halisi na maasumu.

Mbwa wa Mwana Mfalme


Kuna hadithi ya kale ya Kiwelishi kutoka katika karne ya 13 kuhusu mwana mfalme ambaye alirudi nyumbani na kumpata mbwa wake hakitiririkwa na damu usoni mwake. Huyu mtu akakimbia ndani na, kwa kushituka, akaona kwamba mvulana mchanga wake hakuwepo na susu yake ikiwa umependuliwa. Kwa ghadhabu mwana mfalme akauchomoa upanga wake na kumuua mbwa wake. Muda mfupi baadaye, akasikia kilio cha mwanawe—mtoto alikuwa hai! Kandoni mwa mtoto mchanga alilala mbwa mwitu aliyekufa. Yule mbwa, kwa kweli, alikuwa amemlinda mtoto wa mwana mfalme kutoka kwa mbwa mwitu muuaji.

Ingawaje hii hadithi ni ya tamthiliya, inaonyesha jambo fulani. Inaonyesha uwezekano kwamba hadithi hii unatuambia kuhusu kwa nini wengine wanatenda kwa njia fulani kila mara haiambatani na sababu—ambazo wakati mwengine sisi hata hatutaki kujua sababu. Tungependa afadhali tuhisi kujihalalisha wenyewe katika ghadhabu yetu hata kwenye uchungu wetu na maudhi. Wakati mwengine hiki kinyongo kinaweza kuwa kwa miezi au miaka. Wakati mwengine kinaweza kuwa kudumu maisha.
Familia Iliyogawanyika

Baba mmoja hakuweza kumsamehe mwanawe kwa ajili ya kupotoka kutoka kwa njia aliyokuwa amemfunza. Huyu mvulana alikuwa na marafiki ambao baba yake hakupendelea, na alifanya mambo mengi kinyume na kile baba alifikiria alifaa kufanya. Haya yalileta ugomvi kati ya baba na mwana, na huyu mvulana punde alipojiweza, alihama nyumbani na asirudi kamwe.

Hawakuongeleshani tena.
Je! Huyu baba alihisi kujihalalisha? Labda
Je! Huyu mwana akihisi kujihalalisha? Labda

                                Baba, Mama na watoto
Yote ninayojua ni kwamba hii familia iligawanyika na haikuwa na furaha kwa sababu baba wala mwana hakuweza kusamehe mwenzake. Hawangeweza kuona zaidi ya kumbukumbu chungu walizokuwa nazo kuhusu kila mmoja. Walijaza mioyo yao na ghadhabu badala ya upendo na msamaha. Kila mmoja alijinyima nafasi ya kuathiri maisha ya mwenzake kwa wema. Mgawanyiko kati yao ulionekana kuwa wa kina na mpana sana kwamba kila mmoja akawa mfungwa kiroho katika kisiwa chake mwenyewe cha mhemko.

Kwa bahati nzuri, Baba yetu wa Milele aliye Mbinguni mwenye upendo na hekima alifanya njia ya kushinda ufa huu wa kiburi. Upatanisho mkuu na usio na mwisho ni tendo kuu la msamaha na suluhu. Uzito wake ni zaidi ya uelewa wangu, lakini nashuhudia kwa moyo na nafsi yangu yote juu uhalisi na uwezo wake wa msingi. Mwokozi alijitoa Mwenyewe kama fidia ya dhambi zetu. Kupitia Kwake sisi tunapata msamaha.