Monday, 10 March 2014

HADITHI YA UPINDE WA MVUA



Hapo zamani za kale, rangi zote duniani zilianza kugombana, kila moja ikidai kwamba ni bora, muhimu, na yenye matumizi bora yanayopendwa. Mazungumzo yao yalikuwa kama ifuatavyo:
Kijani   Alisema kwa ufasaha;
                "Mimi ni muhimu zaidi. Mimi ni ishara ya maisha na matumaini. Nilichaguliwa kutumika      katika majani, majani ya miti, bila mimi wanyama wote watakufa. Angalia nchi nzima na utaona kwamba mimi ndio niko maeneo mengi zaidi"
Bluu Akaingilia;
                "Wewe unafikiria juu ya dunia tu, angalia anga na bahari. Ni maji ambayo ni msingi wa uhai   na yanatokana na mawingu kutoka kwenye anga. Anga hutoa nafasi, amani na shwari. Bila ya amani yangu nyote mngekuwa si kitu ila kuhangaika tu".
Njano Akahamaki;
                "Wote hamko makini, naleta kicheko, tabasamu na uchangamfu katika ulimwengu huu. Jua, mwezi una rangi ya njano na nyota zote zina rangi ya njano. Kila wakati mkiangalia ua la alizeti, ulimwengu wote unaanza kutabasamu. Bila mimi kuwepo, kusingekuwepo na burudani".
Rangi ya chungwa Alianza kwa kupuliza tarumbeta lake.
                 "Mimi ni rangi ya afya na nguvu. Naweza kuwa adimu, lakini muhimu sana kwa kuwa nina mahitaji yote muhimu ya binadamu. Ninavyo virutubisho vyote muhimu. Hebu fikiria karoti, maboga, machungwa, maembe pamoja na mapapai ! Muda wote sihangaiki, lakini ninapojaza anga asubuhi na jioni uzuri wangu huamsha hisia kiasi kwamba hakuna mtu anayefikiria yeyote kati yenu".
Nyekundu Hakuweza kuvumilia. Alitoa sauti!
                 "Mimi ni mtawala wa vyote, damu na damu ya uhai, mimi ni rangi ya hatari na jasiri! Niko tayari kupigana kwa lolote. Naleta Uhai katika damu, bila mimi dunia ingekuwa tupu kama mwezi. Mimi ni rangi ya hisia ya upendo, rangi ya ua la waridi na rangi ya farasi mdogo".
Zambarau/ Urujuani Aliamka na kujinyoosha kwa urefu wake. Alikuwa mrefu na alisema kwa majivuno na kujigamba;
               "Mimi ni rangi ya uwezo na utawala. Watawala na Maaskofu mara nyingi wamenichagua mimi kuwa mimi ni ishara ya mamlaka na hekima na busara. Watu hawaniulizi mimi, wananisikiliza na kutii."
Nili (Bluu iliyoiva) Aliongea kwa upole zaidi kuliko wenzie lakini kwa kujiamini.
            “Nifikirie mimi. Mimi ni rangi ya ukimya. Ni vigumu sana kunigundua, lakini bila mimi ninyi nyote mnakuwa wababaishaji. Nawakilisha mawazo na fikra zenu, mwanga hafifu na maji ya kina. Mnanihitaji kwa usawa na kulinganisha kwa sala na amani".
Hivyo, rangi zote zikaendelea kutambiana kila moja ikijiamini kuwa ndio bora zaidi kuliko mwingine. Ugomvi ukaendelea kuwa mkubwa. Ghafla kukatokea radi na muungurumo mkubwa. Mvua ikaanza kunyesha kwa nguvu, rangi zote zikapatwa na hofu, zikakaribiana kwa ajili ya kufarijiana! : Huu ndio mwisho wa hadithi.