Wakulima wa kaya
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ametoa wito kwa serikali
ziwawezeshe wakulima wa kaya kwa kubuni sera zinazoweka mazingira
stahiki kwa usawa na maendeleo endelevu vijijin, katika kuendeleza
ujumbe wa 2014 ambao umetengazwa kuwa Mwaka wa Kilimo cha Kaya.
Hayo
ni katika ujumbe wake kwa kongamano na maonyesho ya kimataifa kuhusu
kilimo cha kaya mjini Budapest, Hungary, ambao umetolewa kwa niaba yake
na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kilimo na Chakula, FAO José Graziano da
Silva.
Bwana
Ban amesema kongamano hilo linatoa fursa ya kutambua mchango muhimu
unaotolewa na wakulima wadogowadogo, jamii za wavuvi na wafugaji katika
maendeleo endelevu na katika kutimiza mkakati wa kutokomeza njaa kupitia
kwa mifumo endelevu ya chakula.
kilimo cha umwangiliaji
Nchi kama Tanzania inahitaji kuweka mkanzo wa uwekezaji katika kilimo hasa maeneo mengi ya vijiji ambayo ni mhimu kwa kutoa ajira kwa wananchi walio wengi, kutoa chakula na kuleta ufanisi katika ukuzaji wa pato la nchi. mfano zaidi ya 80% ya watanzania wanategemea kilimo. "Lishe bora inatokana na uwekezaji katika kilimo"
Kilimo cha Mahindi
Source: Redio ya Umaja Wa Mataifa