Miaka
minne iliyopita, Brian Acton alipeleka maombi ya kazi katika kampuni
kubwa za mitandao ya kijamii za Facebook na Twitter. Kampuni zote mbili
zilikataa kumpa ajira akarudi mtaani. Lakini hakukata tamaa,
akashirikiana na marafiki zake kuanzisha kampuni ya WhatsApp na
ikafanikiwa. Leo, mwaka 2014 kampuni ya Facebook inainunua kampuni ya
WhatsApp kwa dola za Kimarekani bilioni 19. Kuna wakati tunakosa nafasi
tunazoona ndizo mkombozi wa maisha yetu, badala ya kutumia muda mwingi
kuangalia tulipokosa na kujilaumu ni bora kuangalia mbele na kuweka
bidii zaidi, uvumilivu na kujituma. Wakati mwingine wanaokataa
kukusaidia wanakupa nafasi ya kufanikiwa zaidi. Hapana inaweza kuwa
baraka. NA MWAMVITA MAKAMBA.

No comments:
Post a Comment