Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imetoka sare ya bila kufungana na Sudan
(Nile Crodcodile) katika mechi ya kujipima nguvu iliyochezwa leo (Juni 2 mwaka
huu) kwenye Uwanja wa Addis Ababa nchini Ethiopia.
Mechi
hiyo iliyochezeshwa na mwamuzi Bamlak Tessema wa Ethiopia ilikuwa sehemu ya
maandalizi kwa timu zote ambazo wikiendi ijayo zinacheza mechi za mchujo za
Kombe la Dunia. Wakati Stars itakuwa ugenini nchini Morocco, Sudan itacheza
nyumbani dhidi ya Ghana.
Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilicheza vizuri mechi hiyo, hasa
kipindi cha pili ambapo ilifanikiwa kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini
ama washambuliaji walipiga nje au mipira yao kuokolewa na kipa Ehab Abdelfatahh
wa Sudan.
Washambualiji
wa Stars akina Khamis Mcha, Mrisho Ngasa na Amri Kiemba wakiongozwa na John
Bocco walilitia msukosuko mara kwa mara lango la Sudan ambalo lilikuwa chini ya
beki wa kati Nadir Eltayeb ambaye alifanya kazi ya ziada dakika ya 72 kuokoa
mpira uliokuwa ukielekea wavuni.
Stars
katika mechi hiyo iliwakilishwa na Juma Kaseja, Nadir Haroub/Vicent Barnabas,
Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Aggrey Morris, Frank Domayo, Mrisho Ngasa,
Salum Abubakar, John Bocco/Haruni Chanongo, Amri Kiemba/Khamis Mcha na Simon
Msuva/Athuman Idd.
Balozi
wa Tanzania nchini Ethiopia, Joram Biswaro amewataka wachezaji wa Taifa Stars
kuhakikisha wanaipeleka timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Dunia
zitakazofanyika mwakani nchini Brazil.
Timu
inaondoka kesho alfajiri kwenda Morocco kwa kupitia Cairo, Misri ambapo
inatarajia kuwasili Casablanca saa 8 mchana.
Boniface Wambura
Ofisa Habari.
No comments:
Post a Comment