Mkuu
wa tume ya marekebisho ya katiba Tanzania;
Tume
ya Mabadiliko ya Katiba nchini Tanzania, imependekeza wawepo wagombea huru
katika ngazi za uchaguzi mbalimbali nchini humo. Hayo ni miongoni mwa
mapendekezo yaliyotangazwa jijini Dar es salaam na Mwenyeketi wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba wakati wa uzinduzi wa Rasimu ya Kwanza
ya Katiba Mpya.
Jaji
Warioba amesema pia wapo wananchi waliopendekeza kwamba, wagombea huru
waruhusiwe kugombea nafasi zote isipokuwa nafasi ya urais. Jaji Warioba amesema
tume ilipitia maoni hayo na kupendekeza kwamba, wagombea huru waruhusiwe
kugombea nafasi zote kuanzia ngazi ya Mwenyekiti wa Mtaa hadi nafasi ya Urais.
Kadhalika
Jaji Warioba amesema, Tume pia imependekeza kwamba, mgombea yeyote wa urais ili
athibitike kuwa ni mshindi atalazimika kupata zaidi ya asilimia hamsini ya
kura, na kwamba endapo mgombea hatafanikiwa kupata asilimia hamsini uchaguzi
utarudiwa kwa kuangalia wagombea wawili waliopata kura nyingi.
Mapendekezo
mengine yaliyotangazwa na Tume ni pamoja na kuwepo kwa serikali tatu yaani ya
Bara,Zanzibar na ile ya Shirikisho.
Pia
tume imependekeza kuwa, Bunge la Muungano liwe na jumla ya Wabunge 75, hamsini
kutoka Bara, ishirini kutoka visiwani na watano wateuliwe na Rais kutoka
makundi maalum ya walemavu.
Mapendekezo
mengine ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ni pamoja na Rais kubakia na madaraka
yake ya uteuzi wa viongozi wa ngazi za juu, lakini uteuzi wa ngazi za chini
uachiwe Tume ya Utumishi.
Imeeleza
kwamba, Rais mara baada ya kufanya uteuzi wa viongozi wa ngazi za juu wakiwemo,
mawaziri, manaibu waziri, jaji mkuu na naibu jaji mkuu, viongozi hao watalazimika
kuthibitishwa na Bunge.
No comments:
Post a Comment