Wachezaji Ame Ally, Kipre Tchetche na John
Bocco wanataraji kuanza katika safu ya mashambulizi ya Azam FC wakati itakapo
wavaa Yanga SC katika mchezo wa Robo fainali ya michuano inayoendelea ya Cecafa
Kagame Cup 2015.
Timu hizo bora zaidi katika soka
Tanzania Bara zitakutana kwa mara ya pili katika michuano hiyo. Mara ya mwisho
zilikutana katika mchezo wa Fainali miaka mitatu iliyopita na Yanha walishinda
kwa mabao 2-0 katika mchezo wa fainali na kutwaa ubingwa wao wa Tano. MECHI YA
LEO..... Azam FC haijaruhusu goli lolote huku ikiwa imeshinda michezo yote mitatu
iliyopita na kufunga mabao Tisa, wakati wapinzani wao Yanha wanaingia katika
mchezo wa leo wakitoka kushinda michezo mitatu ,mfululizo.
Yanga imepoteza mchezo mmoja kati
ya minne iliyokwisha cheza katika hatua ya makundi. Ikiwa imetoka kundi gumu
zaidi katika michuano ya mwaka huu, mabingwa hao mara mbili mfululizo wa zamani
wangependa kuungana na Al Khartoom na Gor Mahia ambazo tayari zimefuzu kwa nusu
fainali.
Timu hizo za Sudan Kaskazini na
Kenya zilikuwa kundi A pamoja na Yanga. BOCCO, AME & KIPRE Walinzi wa Yanga
watakutana na washambuaji wa ' daraja la juu Afrika Mashariki na Kati'.
Kipre tayari amefunga mabao
Matatu katika gemu tatu zilizopita, wakati Bocco amefunga mara mbili. Nyota hao
wawili wamekuwa wakiifunga Yanga mara kwa mara na wanaweza kufanya hivyo kwa
mara nyingine Jumatano hii na kuipeleka timu yao nusu fainali. Nahodha wa
Yanga, Nadir Haroub na ' patna wake' Kelvin Yondan walionekana kupata shida
sana wakati walipokutana na GOR ambayo ilikuwa ikipanga na kufanya mashambulizi
ya uhakika siku ya ufunguzi na walionekana ' kuteswa-kimtindo' na kinara wa
mabao katika michuano hii, nahodha wa Al Khartoum, Salh Eldin katika mchezo wa
mwisho wa hatua ya makundi ambao walishinda 1-0.
Joseph Zuttah na Mwinyi Hajji
wamecheza vizuri hadi sasa, walinzi haoo wa pembeni-Kulia na Kushoto
watalazimika kucheza vizuri zaidi wakati watakapoikabili safu ya mashambulizi
ya Azam FC.
Zuttah amekuwa akipandisha timu kwa
mashambulizi ya uhakika akitokea upande wa kulia, Wakati Mwinyi amekuwa imara,
mwepesi na mwenye pasi za uhakika katika beki mbili. Wawili hao ambao
wamechukua nafasi za Juma Abdul na Oscar Joshua wameifanya safu ya ulinzi wa
kati kuwa na utulivu.
Yanga watashambulia kama kawaida
yao na watatumia zaidi sehemu za pembeni ili kufikisha mipira mbele kwa k uwa
eneo la katikati ya uwanja linataraji kuwa ' gumu' kupitisha mipira kutokana na
aina ya wachezaji ambao watacheza sehemu hiyo.
Jean Mugiraneza, Salum Abubakary
na Himid Mao wanaweza kuanzishwa kama viungo watatu wa Azam FC, wakati, Mbuyu
Twite, Haruna Niyonzima na Deus Kaseke wanaweza kuanza katika nafasi ya kiungo
upande wa Yanga.
Azam wamekuwa wakitumia nguvu zaidi katika
idara nyingi lakini wachezaji wao wa nafasi ya kiungo ni wagumu huku pia wakiwa
na ufundi wa kumiliki mpira.
Niyonzima amekuwa akitawala sana
mechi dhidi ya Azam FC na safari hii atakutana na nahodha msaidizi katika timu
yake ya Taifa ya Rwanda, Mugiraneza. Tutaona mpira wa hali ya juu kama
wachezaji hawatachezeana rafu za ubabe. TAMBWE, NGOMA & BUSUNGU,
Washambuliaji hao watatu wataanza kwa pamoja katika safu ya mashambulizi ya
Yanga. Tambwe amefunga magoli mawili, Busungu amefunga mara tatu wakati, Ngoma
bado anatafuta goli lake la kwanza klabuni Yanga. Washambuliaji hao watatu
wanaweza kufunga hata magoli mawili na zaidi katika gemu moja na kufanya hivyo
mbele ya safu ya ulinzi ambayo haijaruhusu goli lolote katika gemu tatu
mfululizo itakuwa ni jambo kubwa.
Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni,
Aggrey Morris na Paschal Wawa wamekuwa wagumu kupitika, labda ni kutokana na
aina ya timu walizokutana nazo lakini kiu-alisia, Yanga wanapaswa kupambana
hasa ili kuwa timu ya kwanza kufunga goli dhidi ya Azam katila michuano hii.
Safu yao ya mashambulizi imefunga
magoli lakini bado wanakabiliwa na tatizo la upotezaji wa nafasi rahisi za
kufunga magoli. Wawa amekuwa sababu kubwa ya ubora wa sasa katika safu ya
ulinzi kutokana na uchezaji wake wa nguvu, uhamasishaji huku akiwa si mchezaji
wa kufanya makosa yasiyotarajiwa.
Kapombe tayari amehusika katika
magoli mawili ya timu yake. Mlinzi huyo wa kulia anaweza kuwa tatizo kwa Yanga
kutokana na krosi-pasi zake, ni mchezaji asiyechoka kwenda mbele pale
inapohitajika lakini uchezaji wake huo unaweza kuwa tatizo kwa kuwa, Ngoma si
mchezaji wa kumuachia uhuru sana.
Nyoni ameendeleza kiwango chake
kizuri na hivyo ataendelea kupangwa katika kikosi cha kwanza. Atamkabili,
Kaseke ambaye amecheza kwa kiwango cha juu katika gemu nne zilizopita, wakati
Wawa na Aggrey watakuwa macho kuhakikisha, Tambwe na Busungu hawapati nafasi ya
kufunga. Nani mshindi wa gemu hii?. Ni mechi ngumu ila naipa Yanga asilimia 60
za kushinda kutokana na uzoefu wao wa michuano.
Na Baraka Mbolembole, Dar es
Salaam
No comments:
Post a Comment