Sultani
na mtawala wa Brunei ambaye ni mmoja wa matajiri wakubwa duniani Serikali ya
Brunei iliyo Kusini Mashariki mwa Bara Asia, itaanza kutumia sheria kali za kiisilamu.
Kiongozi
wa nchi hiyo ya kiisilamu ambayo ni jirani na Malaysia ametangaza kuwa sheria
hiyo itaanza kutumika kuanzia wiki hii.
Adhabu
zilizo chini ya sheria za kiisilamu ni pamoja na kuwakata wezi mikono na
kuwapiga mawe hadi kufa watu waliopatikana na hatia ya kushiriki Zinaa.
Sheria
hii itatekelzwa katika awamu tatu katika kipindi cha miaka mitatu. Umoja wa
Mataifa tayari umeelezea wasiwasi wake kuhusu sheria hiyo.
Taifa
la Brunei tayari linafuata sheria kali za kiisilamu kuliko hata nchi jirani
kama Malaysia na Indonesia pamoja na kuharamisha uuzaji na utumiaji wa pombe.
Nchi
hiyo ndogo ilio katika kisiwa cha Borneo,inatawaliwa na Sultan Hassanal Bolkiah
na imepata utajiri wake kutokana na kuuza nje mafuta na gesi yake.
Takriban
nusu ya waisilamu wanaoishi katika nchi hiyo ni raia wa Malaysia.
Sultani
alinukuliwa akitangaza hatua ya kwanza ya kuanza kutumiwa kwa sheria hiyo
akimshukuru Mungu na kuwatahadharisha wananchi kuhusu kuanza kutumika kwa
sheria hiyo.
Sheria
yenyewe itaanza kutumika katika kipindi cha miaka mitatu huku hukumu ya makosa
ya kwanza ikiwa kifungo cha jela pamoja na kutozwa faini.
Katika
awamu ya pili ndipo wahalifu wataanza kukatwa mikono kwa watakaopatikana na
hatia ya wizi , huku awamu ya tatu ikihusu kupigwa mawe wazinifu na
wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Sultani
anayetawala kisiwa hicho ni mmoja wa matajiri wakubwa duniani na tayari
amewaonya watu kukoma kushambulia mipango yake kupitia mitandao ya kijamii.
Mfumo
wa sheria katika mahakama nchini humo ni sawa na ule wa Uingereza.
Umoja
wa Mataifa uliitaka serikali kuchelewesha mageuzi hayo ili kuhakikisha kuwa
sheria hiyo inaambatana na sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu.
source: BBC Swahili