Kula vyakula asili inazidisha miaka ya wagonjwa wa moyo Wanasayansi nchini Marekani wanasema watu waliowahi kupata maradhi ya moyo wanaweza kuishi maisha marefu iwapo watakula zaidi vyakula ambavyo havijapitia viwandani.
Watafiti
walichunguza zaidi ya watu elfu nne waliowahi kupata mshituko wa moyo na
kubaini kuwa wana uwezekano mkubwa wa kuishi miaka tisa zaidi kama watakula
vyakula hivyo .
Vyakula
ambayo havijapitia viwandani vina nyuzinyuzi ambazo tayari imethibitishwa kuwa
husaidia katika kuwezesha binadamu kwenda haja bila matatizo.
Vyakula
ambayo vina nyuzinyuzi hizo ni kama vile matunda, mboga na nafaka.
Hatahivyo
wataalam wanasema watu katika mataifa mengi hawali vyakula hivyo kwa wingi.