Tuesday, 4 March 2014

SERIKALI NA MAENDELEO VIJIJINI



MALAWI
KUTOKA WILAYA YA THYOLO, Malawi,
mmoja wa wanachama 24 wa mpango wa umwagliaji katika wilaya ya Thyolo, shamba la bwana JUSA lina ukubwa wa mita 50 kwa 20. Lakini anasema linampatia kipato cha kutosha kuweza kupata mahitaji ya msingi ya familia yake ya watoto watatu. Anahusisha mafanikio yake na huduma za kilimo za ugani. 
 
                                     Mkulima katika shamba lake

"Bwana Sakaika [mfanyakazi wa ugani wa serikali] anakuja hapa mara kwa mara. Ni kutokana na maelekezo yake tunaweza kufaidika kwa kiasi kikubwa na mashamba haya madogo," anasema.

Yeye ni miongoni mwa wachache wenye bahati.
Lakini wakulima wa Thyolo ni pekee ambao wana furaha. Utafiti wa shirika la kupambana na umaskini la kimataifa la ActionAid, unaonyesha kuwa huduma za ugani, ambazo hutoa ushauri na mafunzo kwa wakulima, zimepungua katika maeneo mengi ya Malawi.  Serikali inakubaliana kuwa huduma za ugani ni duni, lakini inalaumu gonjwa la UKIMWI kutokana na uhaba wa wafanyakazi.
 Mtandao wa Mashirika ya Kiraia katika Kilimo nchini Malawi (CISANET) unasema wakulima wa Malawi walikuwa wakifaidika na msaada kutoka wizara ya kilimo, wakati serikali ilipokuwa mtoaji mkuu wa huduma. Hiyo ilikuwa hapo kabla ya kuja kwa sera za soko huria miaka ya 1980.
Sera mpya, kulingana na mratibu wa kitaifa wa CISANET Victor Mhoni, ziliondoa jukumu la serikali kama mtoaji mkuu wa huduma za ugani. Matarajio ni sekta binafsi kuziba pengo
Serikali ilipunguza kwa kasi kubwa matumizi katika eneo hili. ActionAid inasema kati ya mwaka 1996 na 1998, serikali ilitenga asilimia 67 ya bajeti ya kilimo katika huduma za ugani. Matumizi hayo yameshuka hadi asilimia saba mwaka jana, anasema.

Katika bajeti ya mwaka 2010/11, serikali ilitenga dola milioni 213 kwa ajili ya wizara ya kilimo. Kati ya fedha hizi, mpango wa ruzuku za mashambani unapata dola milioni 133. Kazi ya utafiti na ugani inapata dola milioni 9 – asilimia nne tu ya jumla ya bajeti yote ya kilimo. Fedha zinazosalia zitanunua mahindi kwa ajili ya mpango mkakati wa taifa wa hifadhi ya nafaka.
 
KOSA NI LA BRETTON-WOODS?
Action Aid inalaumu wahisani kama vile Benki ya Dunia kutokana na kuishauri serikali kusitisha kusaidia kilimo. Kutokana na kuingiza kilimo katika sekta ya uchumi badala ya usalama wa chakula, shirika hilo linasema, kumesababisha kupungua kwa huduma za ugani nchini Malawi.

Benki ya Dunia inasisitiza kuwa mchanganyiko wa wafanyakazi wa umma, makampuni binafsi, mashirika ya kiraia na mifumo iliyopo katika ngazi ya jumuiya unapaswa kutoa huduma za ugani.

"Hatimaye, tutaweza kupunguza kushuka kwa huduma ambako kumekuwepo na kuongeza uzalishaji wa mashamba madogo. Mpango huu umefanyiwa majaribio katika nchi nyingine za Afrika na unafanya kazi," anasema Hardwick Tchale, mwanauchumi wa kilimo wa Benki hiyo nchini Malawi.

Ripoti ya Maendeleo Duniani ya Benki hiyo 2008 inatoa wito wa kugawa madaraka katika ngazi za chini ili kuleta maendeleo ya huduma za ugani kwenye kilimo.

Ripoti hiyo inataja nchi za Senegal na Uganda kuwa zimepata mafanikio katika kutumia huduma za ugani na shughuli nyingine zinazohusiana na kilimo. ActionAid inakanusha madai haya ya kile kilichojitokeza nchini Uganda na mahali pengine katika ripoti ya mwaka 2008, chapisho la kurasa 25 linalochambua rikodi za Benki hiyo katika kilimo.
"Katika utendaji, huduma za ugani zinajihusisha kidogo mno na sekta binafsi, lakini pia zinaathirika kutokana na uwekezaji mdogo wa serikali. Na kuifanya kuwa hali mbaya zaidi duniani, ni wakulima ambao wanaoumia," wanaandika waandishi wa ripoti.
 

KUFUATA NJIA ZAKE
Malawi inafaidika na hatua zake baada ya kupuuza Benki ilipoanzisha mpango wa ruzuku kuweka mbegu na mbolea mikononi mwa wakulima wadogo; ikiwa ni pamoja na mvua nzuri, na hii imewezesha kuboresha kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa kilimo.
 
Kwa kulinganisha, afisa mwandamizi katika wizara ya kilimo ya Malawi hana matumaini na mafanikio ya sera ya huduma ya ugani ambayo serikali iliitunga mwaka 2000 kwa kushirikiana na Benki ya Dunia.
 
"Hata kama wakulima wamechukua hatua ya kutafuta ushauri kama ambavyo sera inataka wafanye, hawatakuta wafanyakazi katika wilaya kwasababu hatuna wafanyakazi wa kutosha. Na huwezi kushinikiza sekta binafsi kuingia katika biashara," alisema, akitaka kutokutajwa jina lake kwani haruhusiwi kuongea kwa niaba ya wizara hiyo.
 
ActionAid inasema uwiano kati ya wafanyakazi wa ugani na kaya za wakulima ni 1 kwa kila 3,000, mbali zaidi na shabaha ya serikali ya uwiano wa 1:500.  "Tutatunga sera na kutafiti teknolojia zenye lengo la kuendeleza kilimo chetu," afisa wa wizara aliimbia IPS. "Lakini nadhani tunaacha eneo muhimu mno ambalo litawezesha mipango yote na matokeo ya utafiti. Serikali haiwekezi kwenye ugani. Hakuna haja ya kusubiri hadi kuona mipango ya umwagiliaji kwa wakulima kabla hawajapatiwa huduma."

Alisema wafanyakazi wa ugani waliopo sasa wanapata shida kutokana na kukosekana kwa zana za msingi kama vile pikipiki na baiskeli kuwawezesha kutembelea wakulima katika maeno yao ya kazi. 
                                Njia za uchukuzi katika maeneo ya vijiji

 
                                                          Barabara
KUONGEZA RASILIMALI ZILIZOPO
Akizungumza na IPS wakati wa Jukwaa la Utafiti wa Kilimo Afrika (FARA) mjini Burkina Faso mwishoni mwa mwezi Julai, mkurugenzi mtendaji wa FARA Dk Monty Jones alisema serikali za Afrika zinapaswa kufidiwa kwa kiasi fulani kutokana na kukosekana kwa wafanyakazi na kukosekana kwa usafiri kwa kutumia teknolojia mpya za mawasiliano.

"Afrika kwa sasa inaonekana kuwa na soko la simu za mikononi linalokua kwa kasi zaidi. Inaleta mantiki kwa mifumo yetu ya kilimo kutumia teknolojia hizi katika kubadilisha taarifa za ugani," alisema.

Mfanyakazi wa ugani wa wilaya ya Thyolo Sakaika ana baiskeli na simu ya mkononi. Anahusika na mipango 57 ya umwagiliaji ambayo inahudumia wakulima wapatao 4,000.

"Wakati natembelea mpango mmoja leo hii, inachukua muda mrefu sana kurejea nyuma. Hivyo simu ya mkononi inanifanya kuwasiliana na wakulima," alisema.

Na jitihada zake zinalipa. Enock Mpeni, 48, ni mwenyekiti wa mpango wa umwagiliaji ambao Jusa anafanyia kazi. Amekuwa mkulima wa mahindi katika maisha yake yote lakini anasema amegundua kilimo kina faida zaidi tangu mwaka 2007 wakati alipoanza kutumia huduma za ugani katika mpango huo.

Mpeni alielezea jinsi gani maarifa ya kiasi gani cha nafasi kinapaswa kuachwa kati ya mmea na mmea, idadi ya mbegu kwa kila shimo, lini na ni mbolea gani ya kutumia, na utunzaji mzuri wa kumbukumbu vilimsaidia kuwa mkulima bora.


Kama ilivyo kwa Mpeni, Jusa anapanda mahindi aina ya hybrid kwa kila shimo likiwa umbali wa sentimita 30. Mazao yanakomaa kwa kipindi cha miezi mitatu, na hivyo kuwa na nafasi ya kupanda mara nne kwa mwaka.

Kulingana na Sakaika, shamba la mita 50 kwa 20 linapaswa kuwa na mashimo 5,000 ambayo yanazalisha hadi mahindi 10,000. Jusa anauza mahindi wakati yakiwa bado ni mabichi.
Katika mavuno ya mwisho Juni, Jusa alitengeneza dola 350 kutoka shambani mwake. Mwaka 2008, mwaka wa kwanza wa kuwa katika mpango wa umwagiliaji ambao unampatia msaada Sakaika alipata jumla ya dola 1,600.
Source: Nchini Malawi