Friday, 21 February 2014

WAKATI MWINGINE WANAOKATAA KUKUSAIDIA WANAKUPA NAFASI YA KUFANIKIWA ZAIDI"

Miaka minne iliyopita, Brian Acton alipeleka maombi ya kazi katika kampuni kubwa za mitandao ya kijamii za Facebook na Twitter. Kampuni zote mbili zilikataa kumpa ajira akarudi mtaani. Lakini hakukata tamaa, akashirikiana na marafiki zake kuanzisha kampuni ya WhatsApp na ikafanikiwa. Leo, mwaka 2014 kampuni ya Facebook inainunua kampuni ya WhatsApp kwa dola za Kimarekani bilioni 19. Kuna wakati tunakosa nafasi tunazoona ndizo mkombozi wa maisha yetu, badala ya kutumia muda mwingi kuangalia tulipokosa na kujilaumu ni bora kuangalia mbele na kuweka bidii zaidi, uvumilivu na kujituma. Wakati mwingine wanaokataa kukusaidia wanakupa nafasi ya kufanikiwa zaidi. Hapana inaweza kuwa baraka. NA MWAMVITA MAKAMBA.

Saturday, 2 November 2013

NINI CHA KUFANYA UNAPOTENDEWA MABAYA NA MWENZA WAKO

Ili kuwa na uhusiano wenye amani kuna mambo muhimu ya kufanya. Kwani katika mahusiano kuna changamoto nyingi sana  unaweza kukuta kile anachokizungumza mwenza wako akiwa na wewe huku akikuonyesha mapenzi motomoto, na ukafikiri kuwa unapendwa kuliko kitu chochote lakini kumbe akitoka nje anatenda mambo mengine tofauti  na mabaya kabisa.

Kama kweli unataka amani ni vyema kujifunza kutenda mema. Tafakari na penda kufanya yale ambayo wewe mwenyewe ukiyatenda utayafurahia.Ukweli ni kwamba unaweza kufanya mambo kwa siri ukifikiria mwenzi wako hayajui kumbe yawezekana anajua na yeye akaamua kufanya hivyohivyo tena kwa siri yaani wote mkawa mnadanganyana.Hata kama mwenza wako anafanya mambo mabaya.

 Unachotakiwa kufanya ni kuendelea kumfanyia mazuri na si kutenda mabaya kwa kulipiza kisasi, kwani unapotenda mema yule mtenda mabaya atakosa amani na kuanza kutenda mazuri.Unapokwa katika mahusiano unatakiwa kujiona kama mtu mwenye deni la kumpenda mwenzako daima. KILA JAMBO LINAWEZEKANA NI MAAMUZI TU NA USHIRIKIANO BAINA YA WAPENDANAO.