Tukizungumzia Daraja Bora lenye mvuto wa aina yake
katika nchi zote za Ukanda wa Afrika Mashariki hutaacha kulitaja Daraja la
Kigamboni linalopatikana Dar es Salaam Tanzania pekee lakini kubwa zaidi ndio
Daraja pekee linalopita juu ya maji.
Daraja hilo
limetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya matumizi ya kamba (Cable) kubeba uzito
wa daraja, ambalo linaunganisha jiji la la Dar es Salaam na eneo la Kigamboni
na Kurasini.
Pamoja na kujengwa katika ubora wa hali ya juu,
daraja hili lina jumla ya njia sita yaani njia tatu kwa kila upande, pamoja na
njia mahususi kwa ajili ya waenda kwa miguu na waendesha baiskeli ambayo ina
upana wa mita 2 na nusu (2.5 meters) katika kila pande likiwa na uwezo wa
kupitisha magari yenye uzito usiozidi tani 30.
Watanzania wanajivunia kuwa na daraja zuri, la
pekee Afrika ya Mashariki linalopita baharini lenye kuvutia kutokana na
muonekano wake hasa nyakati za usiku.
Hadi kukamilika kwa ujenzi wake Daraja la Kigamboni
limegharimu kiasi cha dola milioni 135 sawa na shilingi bilioni 283
likitazamiwa kuzinduliwa rasmi Aprli 19 na Rais Dk. John Magufuli.
Mambo
muhimu ambayo madereva na watumiaji wengine wa barabara wanatakiwa kuzingatia
ni:-
1) Kuzingatia sheria ya Usalama Barabarani ikiwa ni
pamoja na kufuata mwendo kasi unaotakiwa ili kuepuka ajali na kuepuka uharibifu
miundombinu ya daraja
2) Kufuata alama za barabarani zilizowekwa katika
‘Interchange’ ya Kurasini ili kwenda kwenye uelekeo sahihi.
3) Kuzingatia alama zilizowekwa kwenye milango
(Toll Gates) ya Kituo cha kulipia tozo (Toll Plaza) ili kuepuka uharibifu wa
miundombinu ya kituo hicho.
4) Madereva na watumiaji wa barabara wengine
watakaosababisha uharibifu wa aina yeyote wa miundombinu ya daraja watatozwa
faini au kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria.
5) Kutunza mazingira kwa kuepuka kutupa takataka
katika eneo la daraja.
Aidha, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
inawataka madereva wa magari ya mizigo wanaoegesha katika barabara ya Nelson
Mandela wakisubiri kuingia bandarini watafute eneo stahiki la maegesho na
kuyaondoa magari hayo kwani hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale
watakaoenda kinyume na agizo hili.
Msongamano wa magari hayo husababisha uharibifu wa
barabara na usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment