Friday, 22 April 2016

Mobisol Na maendeleo Vijijini Tanzania

Ushirikiano kati ya Serikali na taasisi mbalimbali zenye lengo la dhati katika kutatua changamoto na kero mbalimbali katika maisha ya wananchi hasa  vijijini ambayo upatikanaji wa huduma za kijamii kama umeme ni ghali ukilinganisha na kipato chao ni muhimu sana kwa tija na maendeleo ya wananchi. Kama mdau na mtaalamu wa maendeleo vijijini napenda kuipongeza kwa dhati kabisa kampuni ya Mobisol Tanzania ambayo inahakikisha kuna maisha bora na yenye kuleta tija kwa wananchi wa Tanzania 

"Mobisol inatoa nishati safi na salama kwa maelfu ya jamii za vijijini zisizo na nishati ya uhakika"


Kwa mipango yake pamoja na ule wa Serikali yetu tukufu ya awamu ya Tano kupitia wizara ya Nishati na Madini chini ya Waziri Prof Sospeter Muhongo kupitia idara ya Umeme vijijini (REA) hakika tunaiona Tanzania mpya yenye Maendeleo endelevu kuanzia vijijini hadi mjini.
Hebu pitia japo kwa ufupi mafanikio ya Mobisol kwa Tanzania   http://www.mobisol.co.tz/ 
Kampuni ya Mobisol yenye makao yake makuu mjini Berlini nchini ambayo inajihusisha na uzalishaji wa umeme wa jua tayari imewaunganisha wateja wapatao 30,000 nchini Tanzania katika kipindi cha miaka 2 tangia ianze kutoa huduma hizi barani Afrika.
Kasi hii ya ongezeko la wateja wanaotumia umeme nishati ya jua kutoka kampuni hii inadhihirisha kuwa uwekezaji wake unaendana sambamba na kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania za kupunguza tatizo la upatikanaji nishati ya umeme nchini.
Katika kuadhimisha mafanikio ya kufikisha idadi ya wateja 30,000 Mobisol imetoa msaada wa kuinganisha na umeme wa nishati ya jua zahanati ya serikali ya kijiji cha Ngasamo kilichopo Simiyu ambapo anatokea mteja aliyejiunganisha na umeme wa kampuni hiyo akiwa anakamilisha idadi ya wateja 30,000 katika nchi hizi mbili za Tanzania na Rwanda ambako inatoa huduma zake.
Akiongea wakati wahafla ya kutoa msaada huo iliyofanyika katika zahanati hiyo, Meneja Masoko wa Mobisol Bwana Nkora Nkoranigwa amesema kuwa kampuni hiyo imejizatiti kuondoa tatizo la giza nchini na kuaikisha iawapatia wananchi umeme wa nishati ya jua wa uhakika kwa kutumia teknolojia ya kisasa na gharama nafuu.

“Sote tunaelewa kuwa nishati ya umeme inahitajika katika kuleta maendeleo ya haraka na kuwaongezea vipato hususani wakazi wa vijijini.Tutahakikikisa tunaunga mkono jitihada za serikali za kuzalisha na kusambaza umeme kwa kwa wananchi hususani wanaoisi maeneo ya vijijini kwa gharama nafuu ii uwasaidia katika itihada zao za kujiendelea kimaisha” alisema.
Bwana Nkoranigwa alisema umeme ikipatikana utasaidia wananchi kuachana na matumizi ya vibatari na kufurahia matumizi ya vifaa vya kisasa kama jokofu, feni, kuchaji simu na viginevyo na kuwezesha watoto kujisomea katika mazingira mazuri wawapo majumbani na mashuleni hali ambayo itasaidia kuongeza kiwango cha ufaulu katika masomo yao.
30000
Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Bwana Patrick Onyango alishukuru kwa msaada huo na kusema kuwa utawaondolea kero ya kukosa nishati ya umeme waliokuwa nayo kwa muda mrefu na itarahisisha utoaji wa huduma za matibabu kwa wagonjwa na aliahidi kuwa watahakikisha wanatunza vizuri vifaa vya nishati hiyo walivyozawadiwa “Kuna msemo kuwa akufaaye kwa dhiki ndio rafiki wa kweli”. Tunaishukuru kampuni ya Mobisla kwa msaada huu wa kusaidia wananchi wengi” alisema.
Naye Afisa Utawala wa Wilaya hiyo kwa niaba ya serikali alishukuru kwa zahanati hiyo kupatiwa msaada wa nishati na aliongeza kuwa serikali wilayani humo itazidi kuunga mkono wawekezaji wanaokuja na miradi ya kusaidia kuleta maendeleo katika jamii kama ulivyo mradi wa nishati wa Mobisol.
Kwa upande wake mteja wa 30,000 wa kampuni ya Mobisol ambaye alisababisha hafla hiyo kufanyika kijijini hapo na zahanati kupatiwa msaada alisema kuwa amefurahi kuona kampuni memuenzi kwa kuleta msaada wa nishati kwenye zahanati wa kuwanufaisha wananchi wote. Akiwa ni mteja wa umeme unaozalishwa na kampuni hiyo alisema ni wa uhakika na gharama nafuu na unafanya maisha kuwa rahisi na kisasa na kuwataka wanakijiji wajiunge kwa aili ya kuishi maisha ya kisasa na kuweza kuanzisha miradi midogo midogo ya uzalishaji kwa utumia nishati hiyo
Chanzo: http://www.mobisol.co.tz



1 comment:

Unknown said...

500-1000 के नोट बंद होने से चमका गोल्ड, 400 रुपये प्रति ग्राम महंगा
Read more todaynews18.com https://goo.gl/HKU1t0