Siku chache baada ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania
John Pombe Magufuli kuzindua rasmi kituo cha kutoa huduma kwa pamoja cha Rusumo
kilichoko kwenye mpaka wa nchi za Tanzania na Rwanda,maofisa wakuu wa Idara ya
Uhamiaji na Mamlaka ya Mapato (TRA) wameelezea jinsi kituo hicho
kitakavyosaidia kuharakisha utendaji wa kazi na namna kitakavyoiongezea
serikali mapato.
Wakizungumza na ITV kwa nyakati tofauti maofisa hao ambao ni
pamoja na Kaimu Kamishina Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Victoria Lembeli na
Kamishina mkuu wa mamlaka ya Mapato Alphayo Kidata wamesema kituo cha huduma
kwa pamoja kilichozinduliwa kitasaidia kuhakiki taarifa kwa urahisi zaidi na
kwa wakati kwa kuwa shughuli za mpakani zitafanyika kwenye jengo moja na
kitawaondolea usumbufu wasafirisha mizigo waliokuwa wakiupata wa kukaa
muda mrefu kwenye mpaka huo wakati wakisubiri kuhakikiwa kwa mizigo waliyokuwa
wakisafirisha
Chanzo: http://www.itv.co.tz/
No comments:
Post a Comment