Monday, 10 March 2014

UPANGAJI WA MIPANGO TANZANIA KWA MAENDELO ENDELEVU:



Tangu tupate Uhuru mwaka 1961, Serikali ilidhamiria kuwa na upangaji shirikishi katika mchakato wa mipango ya kiuchumi, ili kuwa na mfumo wa upangaji unaotoka chini kwenda juu. Juhudi za serikali za kutekeleza dhamira hii zinaweza kuangaliwa katika hatua mbalimbali zilizochukuliwam kushirikisha Jamii katika kujiletea maendeleo yao. Juhudi hizi zinaweza kuangaliwa katika awamu

                      kuu tatu:

  • ·         Kipindi cha 1961 – 66 (Mara baada ya Uhuru)
  • ·           Kipindi cha 1967 – 92 (Azimio la Arusha)
  • ·        Kipindi cha 1992 – 2002 (Kipindi cha Maboresho)


Kipindi cha tatu, 1992 – 2002 kilitawaliwa na maboresho ya sekta ya Umma. Serikali ya Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania (Bara) ilifanya maboresho kwa ajili ya kuongeza ufanisi na uwezo wa
sekta ya umma katika utoaji huduma bora. Maboresho yamejikita katika maeneo yafuatayo:

  • Maboresho ya Utumishi katika serikali kuu
  • Maboresho ya serikali za mitaa
  • Maboresho katika sekta ya fedha
  • Maboresho katika sekta ya sheria
  • Maboresho katika upangaji mipango na baajeti
  • Maboresho katika mashirika ya Umma
  • Maboresho ya muundo wa Tawala za Mikoa


Shabaha za maboresho haya ni kuleta mabadiliko ya majukumu ya serikali kuu kutoka yale ya serikali hujihusisha moja kwa moja na utekelezaji, uzalishaji mali na utoaji huduma na kuwa yale
ya kuandaa sera, kuratibu, kushauri, na kujenga uwezo wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, watu binafsi na mashirika yasiyo a siserikali. Aidha, kujenga mazingira yanayowezesha serikali na wananchi kushirikiana kuboresha utendaji wa kazi kwa upande mmoja na serikali za mitaa kuwa na majukumu ya utekelezaji na usimamizi wa shughuli zote za maendeleo, utoaji huduma, utawala wa kisheria na uimarishaji demokrasia ili kurahisisha maendeleo ya wananchi.

Ingawa serikali iliendelea kuweka mazingira mazuri ya ushirikishwaji kama ilivyoelezwa hapo juu bado ushirikishwaji wa wananchi katika kupanga na kutoa maamuzi uliendelea kumilikiwa na Maafisa mipango / wachumi, warasimu na wafadhili ambao wana hisia potofu za udhibiti na
ufanisi wenye msingi wa “tunajua (wataalamu) wao (Jamii) hawajui” kwa hiyo, Ushirikishwaji wa wananchi katika kupanga na kutoa maamuzi haukutekelezwa kikamilifu. Huko nyuma wananchi walihusishwa tu kwa kutumia njia zifuatazo; (1) Chakula kwa kazi, (2) Kuchangia gharama, (3) Mikataba na walengwa.


Kumekuwepo na majaribio mbalimbali ya kutumia mbinu shirikishi katika baadhi ya maeneo hapa nchini, hasa katika miradi iliyofadhiliwa na wahisani. Baadhi ya mbinu shirikishi zilizotumika katika jitihada hizi ni: PRA, SARAR, ZOOP na LEPSA.

Kwa kiwango fulani mbinu hizi shirikishi zimewezesha Jamii kufanya maamuzi katika mchakato wa upangaji. Hata hivyo mbinu hizi zote zilikuwa zikiegemea zaidi katika kubaini matatizo hivyo basi kuongeza mategemeo ya Jamii kwamba watapewa misaada mara moja kutoka nje kutatua
matatizo yao. Hali hii inajenga tabia tegemezi, pia mara nyingi miradi ya wafadhili inayotumia
mbinu shirikishi inakuwa tayari inayo malengo yao tofauti na yale yanayoibuliwa na wananchi;
hivyo kutoa nafasi ndogo sana kwa Jamii kujiamulia yale wanayotaka.

Kwa mapungufu hayo, juhudi hizi ziliishia kwenye kuwahusisha tu wananchi badala ya kuwashirikisha, kwa ujumla upangaji mipango nchini Tanzania umeendelea kubaki kuwa ule wa
kutoka juu kwenda chini tofauti na mategemeo ya serikali.

Matarajio ya Serikali katika kuimarisha upangaji yalikuwa kama ifuatavyo;-

  1. ·         Kuongeza ushiriki wa wananchi
  2. ·         Kuwa na mipango ya uwiano
  3.       Kuwa na upangaji wa kutoka chini kwenda juu


Mfumo wa upangaji mipango shirikishi wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo unatoa njia ambayo itasaidia serikali kufikia matarajio haya.