Benki ya dunia imebana msaada wa
dola milioni 90 kwa Uganda , siku chache tu baada ya Rais Yoweri Museveni
kuishinisha sheria mpya dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.
Benki hiyo imesema kuwa inataka
kufanya tathmini yake kuhakikisha kuwa malengo yake ya maendeleo nchini Uganda
katika sekta ya afya, ambayo msaada huo ulikuwa unanuiwa, hayataathirika .
Sheria iliyoidhinishwa na Rais
Yoweri Museveni, ilitiwa saini Jumatatu na inatoa adhabu kali kwa watu
wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Wafadhili wengine tayari wameanza
kusitisha misaada Uganda. Wahisani kama Denmark na Norway wamesema kuwa
wataanza kufadhili mashirika moja kwa moja badala ya serikali.
Aslimia 20% ya bajeti ya Uganda
inategemea michango ya wafadhili.
Mpaka sasa nchi tatu za Ulaya
zimeamua kukata misaada yao kwa mamilioni ya dola.
Wizara ya fedha ya Uganda imesema
inasubiri mawasiliano rasmi ya nchi husika, na iko tayari kukabiliana na athari
za hatua hiyo.
Hadi kufikia sasa Waziri wa Fedha Wa
Sweden, akiwa mjini Kampala, alisema waekezaji kutoka nchi yake watakuwa na
wakati mgumu kuweka pesa zao nchini Uganda kwa sababu watakuwa na hofu kuwa
sheria yo yote inaweza kupitishwa kuwadhulumu watu.
Jana serikali ya Uholanzi ilisema
itazuia kwa muda misaada kwa Serikali ya Uganda. Norway na Denmark pia
zimetangaza kupunguza au kusimamisha kwa muda misaada yake kwa Uganda.
Source: BBC Swahili 2014
No comments:
Post a Comment